Habari za Kijamii

TALGWU Msaidieni Mfanyakazi kabla na Baada ya Utumishi wake- Jafo

Waziri wa Nchi OR TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo, akitoa hutuba yake kabla ya kuzindua zoezi la uuzaji wa hisa za TALGWU Microfinance Limited Company TMF PLC kwenye ukumbi wa LPF jijini Dodoma

Na. Atley Kuni- OR TAMISEMI 

Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Seleman Jaffo amezindua zoezi la uuzaji hisa za (TALGWU Microfinance Public Limited Company TMF PLC) na kukiagiza chama hicho cha wafanyakazi katika Mamlaka ya serikali za Mitaa kuboresha na kuendeleza hali nzuri ya wanachama wakiwa kazini na hata baada yakumaliza utumishi wao wa umma.

Akizindua uuzaji huo wa hisa  Waziri Jafo alisema, vipo baadhi ya vyama vya wafanyakazi lakini sio TALGWU bila kuvitaja kwa majina kwamba vimekuwa vikichangisha michango ya wananchama wao na fedha zote kuishia kwenye uendeshaji wa ofisi huku maslahi ya mfanyakazi yakiendelea kuwa duni.

“Naomba niwapongeze TALGWU kwa hatua hii mliyoipiga hata kuwa na taasisi yenu itakayo kuwa mkombozi kwa mfanyakazi hata baada ya kukoma kwa utumishi wa umma, vipo baadhi ya vyama vya wafanyakazi vyenyewe badala yakuhangaika na kubuni miradi itakayo wasaidia wanachama wake vimekuwa vinara vya kuandaa migomo lakini sio ninyi” alisema Waziri Jafo.

Waziri Jafo alisema mbali na kuuza hisa chama hicho kifikirie mbali zaidi namna sehemu ya michango ya wanachama itakavyoweza kukatwa   na kumnunulia mwanachama hisa moja kwa moja badala ya fedha zote zinazo katwa kupelekwa kwenye matumizi ya ofisi.

Waziri Jafo aliwatoa hofu wanachama hao na kuwataka kujitokeza kwa wingi kununua hisa kwakuwa katika soko la hisa jinsi zinavyo nunuliwa kwa wingi ndivyo na ongezeko la gawio linavyo kuwa kubwa.

“Niimani yangu katika shghuli hii ya leo kila mshiriki amepata na kuusoma waraka wa matarajio ya TMF PLC ambao bila shaka yoyote utamwezesha kila mmoja wenu kufanya maamuzi ya kununua hisa kutokana na uwezo na taratibu zilizo wekwa” alisema Waziri huyo Mwenye dhamana na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Akitoa taarifa ya mwenendo wa TALGWU Micro Finance Limited Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Jackson Ngalama alisema hadi kufikia 2017 mali za TALGWU Micro finance zilifikia thamani ya Tsh. 7.4 bilioni huku faida ghafi ikiongezeka kutoka 44.6 na kufikia 730 Milioni

Ngalama alisema kutokana na uwekezaji uliokwisha fanyika hadi sasa jumla ya wanachama 4,474 walikwisha nufaika na mikopo hadi kufikia mwaka 2017 ikilinganishwa na wanachama wa TALGWU 58,000 ambao ni asilimia 7.7 ya wananchama wote.

TALGWU Microfinance Limited inatazamia kuuza hisa zitakazo wawezesha kupata kiasi cha Tsh.6.3  bilioni ambazo zinatazamiwa kuuza hisa milioni sita na elfu thelasini na saba.

Burudani ikiongozwa na Balozi wakutangaza TALGWU Micro Finance

Mkurugenzi wa TALGWU Micro Finance Limited Company akisoma taarifa ya taasisi hiyo Jackson Ngalama
Hapa sasa ndio uzinduzi wa hisa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *