Afya

TAMISEMI na Wizara ya afya Kuboresha takwimu za mifumo sekta ya afya

Na Fred Kibano

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Zainab Chaula ameongoza kikao kazi kati ya Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuhusu utengenezwaji wa mtandao wa takwimu za Sekta ya afya na mapitio ya mkakati wa uimarishaji ufuatiliaji na tathmini katika sekta ya afya.
Dkt. Chaula amesisitiza matumizi ya takwimu sahihi ili kuboresha sekta hiyo muhimu nchini.
Baadhi ya washiriki wamesema takwimu za afya zitasaidia kujua hudumazinazotolewa ikiwa ni pamoja na kuwatambua wadau wote wa afya kazi wanazozifanya, mahali walipo, bajeti zao, taarifa zao muhimu na mambo mengine katika sekta ya afya.
Aidha imeelezwa kutakuwepo na mafanikio makubwa zaidi katika sekta ya afya endapo kutakuwa na mfumo mama ambao utaongea pamoja na mifumo mingine kama ilivyo kwa mfumo wa epicor 10.2 na mifumo mingine ya GotHomis na mingineyo.
Ofisi ya Rais TAMISEMI inafanya maboresho mbalimbali kwa kushirikiana na wizara za kisekta na wadau ili kuboresha huduma kwa wananchi.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Zainab Chaula akisikiliza jambo wakati wa majadiliano ya kikao kazi cha kutengeneza mtandao wa takwimu kaati ya Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizra ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Jijinoi Dodoma leo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *