Video

TAMISEMI Yaendelea Kuboresha Utawala Bora Katika Mikoa na Halmashauri

Na. Fred Kibano

Dkt. Andrew Komba Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Kisekta Ofisi ya Rais TAMISEMI, ameongoza wajumbe wa Warsha ya Mkakati wa UNICEF kusaidia Ugatuaji wa Madaraka na masuala ya Utawala Bora katika ngazi ya Serikali za Mitaa nchini kwa pamoja kati ya Wadau kutoka UNICEF, Idara ya Uratibu wa Kisekta Ofisi ya Rais TAMISEMI na Menejimenti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI imefanyika katika makao makuu ya Ofisi ya Rais TAMISEMI mjini Dodoma.

Warsha hiyo ina lengo la kujua hali halisi ilivyo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, changamoto zake na kuona namna ya kuboresha masuala ya utawala bora katika kipindi cha miaka ya 2018, 2019, 2020 na 2021.

Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ipo kikatiba ambapo Sura ya nane, Ibara ya 45 inataja kuwepo kwa wizara hiyo. Aidha, kuwepo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kama inavyoelezwa katika Ibara ya 146 ni kuwapa mamlaka watu ili kuamua mambo wanayoyataka yafanyike kwa mujibu wa mahitaji yao.

Mwaka 2015 Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliihamisha wizara ya TAMISEMI kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na kuwa chini ya uangalizi wake ambapo wizara inakuwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI mmoja na Naibu Mawaziri Ofisi ya Rais TAMISEMI watakaoteuliwa naye, Pia Mheshimiwa Rais ndiye Waziri kamili.

Sera ya Ugatuaji wa Madaraka kwa Umma kitaifa inasimamiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) na katika hatua nyingine wizara za kisekta kama wizara ya Maji, Afya, Ardhi, Uvuvi na Mifugo watatunga Sera na miongozo ambayo utekelezaji wake unafanywa na Ofisi ya Rais TAMISEMI katika ngazi ya Wizara, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Ofisi ya Rais TAMISEMI inasimimia Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa upande wa Tanzania Bara. Mpaka kufikia mwaka huu nchini, Tanzania Bara kuna mikoa 26, wilaya 139, Halmashauri 185, tarafa 562, kata 3,963 mitaa 4,037 vijiji 12,545 na vitongoji 64,677.

Baadhi ya wana Warsha ya Mkakati wa UNICEF kusaidia Ugatuaji wa Madaraka na masuala ya Utawala Bora katika ngazi ya Serikali za Mitaa Tanzania Bara wakijadili jambo wakati wa warsha hiyo ofisini Ofisi ya Rais TAMISEMI mjini Dodoma leo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *