Habari za Wizara

Timu ya Mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kushiriki ligi ya Muungano Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na timu ya mpira wa pete ya TAMISEMI leo mara baada kuiaga timu hiyo ambayo inashiriki michuano ya Ligi ya Muungano Zanzibar 2019 inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Na. Majid Abdulkarim

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo ameitakia kila la heri Timu ya Mpira wa Pete ya TAMISEMI inayokwenda kushiriki michuano ya Ligi ya Muungano Zanzibar 2019 na kuitaka kurudi na ushindi katika michuano hiyo.

Mhe. Jafo ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati wa kuiaga timu hiyo ambayo inategemea kusafiri kuelekea Visiwani Zanzibar kwa ajili ya kushiriki Michuano ya Ligi ya Muungano Zanzibar 2019 ambayo inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

“Ninaomba muwe na nidhamu kwa kuwa ni jambo la msingi katika kufanikiwa, michuano hii ni muhimu na mnatakiwa kulinda heshima na nidhamu ya Wizara,” amesisitiza Mhe.Jafo

Aidha Mhe.Jafo amesema kuwa ili timu hiyo ifikie malengo  na kupata ushindi inatakiwa kujenga ushirikiano, umoja  na  kuheshimu maelekezo  yanayotolewa na mwalimu pamoja na viongozi wa timu waliyoambatana nao.

“Naimani kuwa timu ya OR-TAMISEMI ni bora na inauwezo wa kufanya nyema katika michuano hiyo tukafanye vizuri kwa kuwa uwezo upo na ushindi utapatikana,” ameongeza Mhe.Jafo

Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Mhandisi Joseph Nyamhanga ameitaka timu hiyo kutumia uwezo walionao katika kupata ushindi  katika michuano ya Ligi ya Mapinduzi Zanzibar 2019 ili kujenga heshima  Ofisi ya Rais -TAMISEMI.

Mhandisi Nyamhanga ametoa shukrani kwa wachezaji na viongozi wa timu hiyo kwa juhudi na mafanikio wanayopata katika kuitumikia timu hiyo.

Baadhi ya Wachezaji wa Timu ya Mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo leo wakati alipokuwa akitoa nasaha zake kabla ya timu hiyo kusafiri kuelekea Visiwani
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo akizungumza na wachezaji wa Timu ya Mpira wa Pete wa TAMISEMI (hawapo pichani) leo wakati wa kuwaaga kabla ya timu hiyo kusafiri kuelekea Visiwani Zanzibar kushiriki Michuano ya Ligi ya Muungano Zanzibar 2019 inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *