Habari za Wizara

Timu za uendeshaji wa Hudama za afya Mkoa na Wilaya zatakiwa kuwa wabunifu

Naibu Katibu Mkuu Afya, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dkt.Dorothy Gwajima akiwaonyesha moja ya taarifa ya utekelezaji majukumu kwa Timu za huduma za afya Mkoa (RHMT) na Wilaya(CHMT),(hawapo pichani) katika kikao cha Mrejesho wa Utekelezaji wa yatokanayo na ziara za usimamizi shirikishi za utendaji kwa watoa huduma za afya katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino leo Jijini Dodoma kilichofanyika leo katika ukumbi wa Reforms uliopo katika Ofisi ya Rais, TAMISEMI.

Na. Majid Abdulkarim

Kamati za huduma za afya Mkoa (RHMT) na Wilaya (CHMT) nchini zimetakiwa kuwa wabunifu katika kutekeleza shughuli zake na kuhakikisha wanaboresha huduma za afya kuanzia ngazi ya msingi hadi Mkoa kwa ujumla ili kuleta matokeo bora kwa watanzania.

Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu Afya, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dkt.Dorothy Gwajima katika kikao cha mrejesho wa utekelezaji wa yatokanayo na ziara za usimamizi shirikishi za utendaji kwa watoa huduma za afya katika Halmashauri ya Jiji  la Dodoma na Halmashauri ya Chamwino leo Jijini Dodoma kilichofanyika katika Ofisi ya Rais, TAMISEMI.

Kikao hicho ni mwendelezo wa mkakati maalumu wa kuzifunda timu za uendeshaji huduma za afya Mikoa na Wilaya kwa kuanzia na Mkoa wa Dodoma ili,ziweze kufanya uwajibikaji wenye matokeo na kuwaridhisha watumiaji wa huduma za vituo vya tiba na kuwa mfano wa kuigwa na Mikoa mingine” be the center of excellence”.

Dkt. Gwajima amesema kuwa, ubunifu unaotakiwa ni kujenga mahusiano mazuri baina ya mteja na mtoa huduma za afya ili, mteja aweze kuwa uhuru na kujisikia faraja katika kupata huduma kutoka kituoni hapo.

Amesema ni muhimu kuweka mkazo katika eneo la kitabibu na kuhakikisha kuwa, huduma hizo ni sahihi, salama na rafiki kwa vigezo vyote na wateja wanaridhika nazo.

“Mahusiano mazuri yanajengwa na ukarimu, lugha nzuri kwa mteja na umahiri wa utendaji kazi wenu wa kitaaluma kwa ujumla wakati wa kuwahudumia wateja wenu kwa kuwa wateja waliohudumiwa vizuri ndiyo ambao mawakili wazuri katika jamii yao kulingana na jinsi ambavyo wamefurahia huduma zenu” Amesema Dkt.Gwajima

Dkt.Gwajima amewaagiza  watoa huduma za afya kuwa na mpango kazi utakaoweza kuwaongoza vyema katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku na kuweza kupimwa juu ya uwajibikaji wao pasipo shaka.

Anaendelea kufafanua kuwa mpango kazi kwa mtumishi utasaidia kuweza kupata tathimini ya utekelezaji wa majukumu ya mtoa huduma za afya na kujua matokeo yapi yamefanikiwa na kubaini changamoto zilizojitokeza na kuzitafutia suluhisho ili kufikia malengo ya mtoa huduma aliyojiwekea katika mpango kazi wake.

“Ili kupata tathimini ya utendaji kazi wa watoa huduma za afya amesisitiza kuhakikisha kila mmoja kuwa na taarfa ya uwajibikaji wake huku ukiwa na takwimu sahihi wakati wote. Ameongezea Dkt.Gwajima

Aidha Dkt.Gwajima amehitimisha kwa kuwataka watoa huduma za afya kutekeleza mipango kazi yao kwa vitendo ili kuweza kupata matokeo chanya yatakayoonyesha mabadiliko katika sekta ya afya badala ya kuwa na watumishi ambao, ukimuuliza utemdaji kazi wa siku anakuwa  hana maelezo yenye takwimu bayana.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt.Samwel Seseja amesema kuwa atasimamia vyema maelekezo yalotolewa  ili kuhakikisha utendaji kazi na uboreshaji wa huduma za afya kuanzia ngazi ya msingi hadi Mkoa zinaboreka na kuimarishwa vizuri kwa faida ya watanzania.

Baadhi ya wajumbe katika kikao cha Mrejesho wa Utekelezaji wayatokanayo na ziara za usimamizi shirikishi za utendaji kwa watoa huduma za afya katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino leo jijini Dodoma kilichofanyika katika ukumbi wa Reforms uliopo katika Ofisi ya Rais, TAMISEMI wakimsikiliza kwa umakini Dkt.Gwajima .
Baadhi ya wajumbe wa timu za huduma za afya Mkoa (RHMT) na Wilaya(CHMT)wakiwa katika kikao cha Mrejesho wa utekelezaji wa yatokanayo na ziara za usimamizi shirikishi za utendaji kwa watoa huduma za afya katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino leo jijini Dodoma kilichofanyika leo katika ukumbi wa Reforms uliopo katika Ofisi ya Rais, TAMISEMI.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *