Habari za Wizara

Viongozi wa Serikali za Mitaa kuweni chachu ya Mabadiliko, Nzunda

 Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri akichangia mada kwenye warsha ya namna ya Uendeshaji wa mabaraza ya Biashara kwa Mikoa na Halmashauri zote nchini iliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Mradi wa Local Investiment Climate (LIC) iliyofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma.

Na. Angela Msimbira OR -TAMISEMI

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  anayeshughulikia Elimu Tixon Nzunda amewaagiza Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kujenga uelewa wapamoja  kwenye ngazi ya Halmashauri na wadau wa Biashara kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali nchini.

Nzunda ameyasema hayo wakati akifunga warsha ya namna ya Uendeshaji  wa mabaraza ya Biashara  kwa Mikoa na Halmashauri zote nchini iliyoandaliwa  na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Mradi wa Local Investiment Climate (LIC) iliyofanyika kwa siku mbili katika ukumbi  wa LAPF Jijini Dodoma.

Nzunda amesema Mamlaka za Serikali za Mitaa hazifanyi kazi kama timu ambapo mpaka sasa wataalamu  wengi hawajui miradi inayotekelezwa na  mradi wa Local Investiment Climate (LIC) utashangaa anayefahamu ni Mkurugenzi tu hali inayopelekea kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.

 “Menejimenti  za Mamlaka za Serikali ya Mitaa bado hazijajua utekelezaji wa mradi wa LIC ambapo ukimuuliza Afisa Kilimo, Mchumi au mweka hazina kuhusu mradi huo wanakuwa hawana manijibu yanayoeleweka” Anasema Nzunda

Nzunda anafafanua kuwa Menejimenti isipokuwa na uelewa wa pamoja katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo haiwezi  kufanya kazi ya kukuza uchumi wa nchi, ni vyema kukawa na uelewa wa miradi hiyo kuanzia ngazi ya Kata, Wilaya, na Mkoa kwa ujumla.

Nzunda amewaagiza Viongozi hao kutoe elimu kwa Menejimenti zao ili kujenga uelewa wa pamoja  kwenye ngazi ya Halmashauri na kwa wadau wa maendeleo kwa kuwa Uwekezaji unafanyika katika ngazi ya  Halmashauri  na pia ni vyema wananchi wapewe elimu  hii  ili wajue  kinachokwenda kutekelezwa kupitia mradi wa LIC.

Amewataka  viongozi hao kubadilisha mtanzamo na tabia ya  kuwaona wawekezaji kama wamekuja kumaliza shida zao ambapo wanachi hawachangii nguvu kazi katika kukamilisha miradi hiyo kinachotakiwa kwa sasa ni  mtizamo chanya wa kushirikiana nao na kuwawezesha kukamilisha miradi hiyo.

Amesema kufanikiwa kwa Wawekezaji hasa wa Sekta Binafsi  kutasaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa  kuweza kupata mapato zaidi  kupitia kwenye uwekezaji unaofanyika nchini.

Amewaagiza Viongozi wa Serikali za Mitaa kukaa pamoja na Wawekezaji na kujadiliana nao  ili waweze kutoa maoni yao ili  Serikali  iweze kupanga mikakati ya pamoja ya namna ya kusonga mbele katika kuimarisha mazingira ya uwekezaji Nchini.

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bi. Rehema Madenge akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia elimu Tixon Nzunda kwenye warsha ya namna ya Uendeshaji wa mabaraza ya Biashara kwa Mikoa na Halmashauri zote nchini iliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Mradi wa Local Investiment Climate (LIC) iliyofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu Tixon Nzunda akisisitiza jambo wakati alipokuwa akifunga warsha ya namna ya Uendeshaji wa mabaraza ya Biashara kwa Mikoa na Halmashauri zote nchini iliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Mradi wa Local Investiment Climate (LIC) iliyofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Files Kibasa akieleza fursa za uwekezaji zinazopatikana Wilayani Kondoa kwenye warsha ya namna ya Uendeshaji wa mabaraza ya Biashara kwa Mikoa na Halmashauri zote nchini iliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Mradi wa Local Investiment Climate (LIC) iliyofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *