Habari za Wizara

Wadau wa afya watakiwa kufanya tathmini na ufuatiliaji

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Zainabu Chaula akikabidhi vyeti kwa washiriki Kongamano la Pili la Ufuatiliaji na Tathmini linalofanyika leo likishirikisha wadau mabalimbali waliwemo wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe na Watafiti lililofanyika katika Ukumbi wa Morena Jijini Dodoma.

 

Na. Angela Msimbira OR- TAMISEMI

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Afya) Dkt. Zainabu Chaula amesema ili kuongeza ufanisi katika kuandaa mipango ya afya nchini ni vyema ufuatiliaji na tathmini ukafanyika ili kuimarisha afya ya jamii na kutoa huduma bora za afya nchini

Dkt. Chaula ameyasema hayo leo  Jijini Dodoma wakati akifunga Kongamano la pili la tathmini na ufuatiliaji lililloandaliwa na Chuo Kikuu Mzumbe kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha California  cha nchini Marekani likilenga kujadili na kuweka mikakati ya namna bora ya kutumia matokeo ya tafiti za sekta ya afya kufanya tathmini na ufuatiliaji ili kuimarisha huduma za afya  zinazotolewa nchini.

“Serikali imekuwa  na programmu, mipango na afua mbalimbali, hivyo tunapokuwa na programmu hizo tunaangalia  matokeo  na mabadiliko hivyo mkutano huu unaelekeza kufanya ufuatiliaji na tathmini katika sekta ya afya ili kuweza kutoa huduma bora kwa jamii,” alisema Dkt Chaula.

Alisema kuwa kwa sasa watu wengi wanapanga mipango mingi pasipo kufanya ufuatiliaji na tathimini ya kina ya kile wanachokitekeleza, hivyo amewaagiza wadau wote wa sekta ya afya nchini kuhakikisha wanafanya tathmini ya kile wanachokifanya ili kupata matokeo chanya na kuona matokeo yaliyopatikana na kujua kama mipango iliyopangwa na Serikali inaendana na matakwa ya wananchi.

Dkt. Chaula alisema kuwa ufuatiliaji na tathmini unawezesha kujua yaliyopangwa kama yamefikiwa kulingana na makubaliano yaliyowekwa na kutimiza malengo ya utoaji wa huduma kwa jamii hasa katika suala  la utoaji wa huduma za afya.

Aidha, Dkt Chaula amekitaka Chuo Kikuu cha Mzumbe  kufanya kazi kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya afya ikiwemo  Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais-TAMISEMI na wadau mbalimbali wanao jishughulisha na masuala ya afya kwa lengo la kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya  afya nchini

Kwa upande wake Bw. Alfred Magala mmoja ya mshiriki wa mafunzo hayo amesema mafunzo hayo yamesaidia kujua mifumo ya ufuatiliaji  ambayo itajenga uwezo  wa watumishi wa afya  na wananchi pamoja na watendaji  katika kufanya maamuzi ya  kisera , kiutawala  na maamuzi ya kiutendaji ambayo yatasaidia kuboresha afya za  wananchi.

Aidha Chuo Kikuu Mzumbe kinatoa elimu na mafunzo katika eneo la ufuatiliaji na tathimini katika sekta ya afya na  sasa kuna programu mbili za shahada ya kwanza na uzamili katika masuala ya afya na kozi fupi fupi kwa ajili ya kujenga uwezo wafanyakazi katika sekta ya afya wanaoshughulika na mfumo.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Zainabu Chaula akiwa katika picha ya pamoja (katikati) na baadhi ya washiriki wa Kongamano la Pili la Ufuatiliaji na Tathmini linalofanyika leo likishirikisha wadau mabalimbali waliwemo wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe na Watafiti lililofanyika katika Ukumbi wa Morena Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Zainabu Chaula akifunga Kongamano la Pili la Ufuatiliaji na Tathmini linalofanyika leo likishirikisha wadau mabalimbali waliwemo wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe na Watafiti lililofanyika katika Ukumbi wa Morena Jijini Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *