Habari za mikoani

Wananchi Bolisa Kupata Shule Mpya

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge kushoto akimuonyesha
kitu Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mh. Sezaria Makota wakati wa wa ukaguzi
wa jengo la ofisi ya kata ya Bolisa

Na: Sekela Mwasubila H/W Kondoa Mji

Tatizo la muda mrefu lakutokuwepo kwa shule katika Kata ya Bolisa Wilaya ya Kondoa huenda likafikia mwisho kufuatia mipango kabambe iliyo tayarishwa na Halmashauri ya Mji Kondoa kuamua kumaliza tatizo hilo.

Mkurugenzi wa Mji Kondoa Khalifa Kondo akifafanua jambo kwenye
mkutano wa wananchi na Mkuu wa mkoa

Akizungumza katika Ziara ya Mkuu wa Mkoa Mkurugenzi wa Mji Kondoa Khalifa Kondo alipokuwa akijibu swali mbele ya Mkuu wa Mkoa wakati wa mkutano wa wananchi wa Kata ya Bolisa na Mkuu wa Mkoa alipofanya ziara ya kujitambulisha wilayani humo hivi karibuni.
Akijibu swali hilo lililo ulizwa na mwannchi, Abubakar Mussa, Kondo alisema, awali kabla ya kugawanywa kwa Kata, ilikuwepo Shule ya Sekondari Gubali, ambayo kimsingi ilijengwa kwa ushirikiano wa wananchi wa kata hizo mbili, lakini baada ya mgawanyo wa mipaka ya kiutawala, jitihada zilizopo mbele ni kujenga shule Nyingine itakayo wahudumia watoto kutoka katika Kata ya Bolisa.
“Wilaya imejipanga kujenga shule mpya ya Sekondari kwa ajili ya wananchi wa kata ya Bolisa kwa ajili ya kuwasogezea huduma wananchi kwa ukaribu kwani ndio lengo la serikali ya awamu ya tano” alisema Kondo.
Sambamba na hilo Kondo aliongeza kuwa Rais amemwagiza Waziri wa ujenzi kuiachia wilaya majengo yaliyokuwa yanatumiwa na kampuni ya ujenzi wa barabara eneo la Kolo ili yatumike kwa ajili ya kuanzisha shule ya sekondari kwa wanafunzi wenye vipaji maalum toka nchi nzima.
Wanafunzi wa shule ya msingi Bolisa wakicheza ngoma ya Kirangi
kwenye mkutano wa wananchi na mkuu wa Mkuu wa Mkoa

Baada ya ufafanuzi huo Mkuu wa Mkoa Dkt. Binilith Mahenge alipongeza mpango huo na kuwataka kuutekeleza kwa ushirikiano ili wananchi wapate huduma inayostahili.
Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dodoma, yupo katika ziara yakujitambulisha katika Wilaya Mbali mbali mkoani hapa mara baada yakuhamishiwa Mkoani humo akitokea Mkoa wa Ruvuma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *