Habari za Kijamii

Waziri Jafo asababisha shangwe kwa wafanyabiashara wa  Mabibo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe.Selemani Jafo akizungumza na wafanya biasra wa Mabibo kwenye Mkutano uliofanyika katika Soko hilo kuhusu mauafaka dhidi ya mgogoro uliopoa baina ya wafanyabisara hao na Kiwanda cha Urafiki.

Wafanyabiashara wa Mabibo wakimskiliza Mhe.Waziri Selemani Jafo(hayupo pichani)

Wafanyabisara wa Mabibo wakifuatilia Mkutano wa Waziri Jafo kuhusu suluhisho la wao kuondolewa katika kiwanja cha Soko hilo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe.Selemani Jafo akizungumza na wafanya biasra wa Mabibo kwenye Mkutano uliofanyika katika Soko hilo kuhusu mauafaka dhidi ya mgogoro uliopoa baina ya wafanyabisara hao na Kiwanda cha Urafiki.

  Wafanyabiashara wa Mabub wakishangilia Tamko la Mhe.Waziri Jafo la kuendelea kufanya Biashara katika eneo hilo mpaka watakapofanya mazungumza na Viongozi wa Kiwanda 

Nteghenjwa Hosseah, Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amekutana na wafanyabiashara wa Soko la Mabibo Jijini Dar es Salaam na kutoa Tamko la Serikal kuhusu wafanyabiashara hao kuhamishwa na kuachia eneo hilo ambalo ni Liko chini ya miliki ya Kiwanda.

Wazii Jafo amesema nimekuja hapa baada ya kupata malalamiko kupitia wa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kwamba mnataka  kutolewa kwa sababu kiwanja hiki sio kiwanja cha Soko halali na Mahakama imetoa hukumu abayo inaonyesha eneo hili liko chini ya Miliki ya Kiwanda.

“Sisi hatuna Mamlaka ya kuvunja hukumu ya Mahakama lakini katika hili kuna maslahi mapana ya wafanyabiashara ambao ni wanyonge wanaofanya biashara katika eneo hili lazima tuwaangalie kwa namna tofauti na kuangalia namna ya kuwasaidia ili waweze kuendesha maisha yao”

Aliongeza kuwa Agenda ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufu ni kuhakikisha wanyonge wanapata haki zao hivyo ameniagiza nije kuwasikiliza na kutafuta suluhisho la haraka dhidi ya wafanyabiashara wa Mabibo.

“Baada ya kufika hapa nimetoa agizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda kukutana na Yono Auction Mart, Uongozi wa Kiwanda na wote wanaohusika ili tupate njia muafaka ya kuhakikisha wafanyabishara wa eneo hili wanaendelea kufanya biashara zao vizur kama walivyokuwa wanafanya hapo awali”.

Naomba muwe watulivu muendelee na biashara zenu, suala hili Serikali inalishughulikia kwa umakini na haraka zaidi ukizingatia hiki ni kipindi cha mwezi January ambapo Fedha zinahitajika kwa ajili ya ada za watoto, kodi za nyumba nk mkibugudhiwa mtashindwa kukidhi mahitaji ya Familia alimalizia Mhe.Jafo.

Soko la Mabibo lenye wafanyabiashara zaidi ya elfu mbili limekubwa na mgogoro huu miezi kadhaa iliyopita kufuatia Kiwanda cha Urafiki kuwataka waondoke hapo ili kupisha eneo hilo kwa matumizi ya kiwanda ilihali eneo maalumu la kuwahamishia wafanyabiashara hao bado halijakamilika lakini pia wafanyabishara wamekuwa wakionyesha hisia zao kuwa eneo hilo walilopo sasa ni la Kimkakati kwa  biashara zao kutokana kuwa katikati ya Mji hivyo kuwa rahisi  kufikika kwa wateja wa aina zote.

Mwisho.